12/06/2026
🔴KISUKARI NA KIHARUSI: UHUSIANO .
💢 Kisukari (Diabetes Mellitus) ni ugonjwa wa muda mrefu unaosababisha ongezeko la sukari kwenye damu kutokana na upungufu wa insulini au mwili kushindwa kuitumia ipasavyo.
💢Kiharusi (Stroke) ni hali ya dharura ya kitabibu inayotokea pale mtiririko wa damu kwenda kwenye sehemu ya ubongo unapoziba (Ischemic Stroke) au mshipa wa damu kupasuka (Hemorrhagic Stroke).
📌AINA ZA KISUKARI:
_Type 1 Diabetes Mellitus
_Type 2 Diabetes Mellitus
_Gestational Diabetes (Kisukari cha ujauzito)
📌SABABU ZA KISUKARI:
•Kurithi vinasaba (genetics)
•Unene kupita kiasi
•Kutofanya mazoezi ya mwili
•Lishe yenye sukari na mafuta mengi
•Matatizo ya homoni na kongosho
📌DALILI ZA KISUKARI:
•Kiu kupita kiasi
•Kukojoa mara kwa mara
•Njaa ya mara kwa mara
•Kuchoka haraka
•Vidonda kupona polepole
📌KISUKARI HUSABABISHAJE KIHARUSI? Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu huharibu kuta za mishipa ya damu na kuongeza uwezekano wa kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo.